Header Ads Widget

HII NI BAADA YA MATOKEO MABAYA KATIKA KOMBE LA DUNIA BALOTELLI AFANYA MATANUZI YA 'SIJALI LOLOTE' MAREKANI NA KIMWANA MKALII



Mahaba matamu: Wawili hao walikula raha sana mjini Miami
BAADA ya matokeo mabaya katika Kombe la Dunia akiwa na timu yake ya taifa, Italia, mshambuliaji Mario Balotelli amepigwa picha akivuta sigara na kufanya matanuzi na mpenzi wake Fanny Neguesha mjini Miami, Marekani.
Mshambuliaji huyo wa Milan, ambaye alipigwa faini na klabu yake kwa kuvuta sigara kwenye treni mwaka jana, haonekani kabisa kuwa na dalili za kuacha sigara baada ya kupigwa picha akiwa kwenye korido la hoteli anavuta.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 yupo mapumzikoni na mpenzi wake, Fanny Neguesha baada ya Kombe la Dunia ambako alifunga bao moja tu dhidi ya England, Italia ikitolewa hatua ya makundi.




Maisha ufukweni: Nyota wa Italia, Mario Balotelli akiwa na mpenzi wake Fanny Neguesha mjini Miami

Kitu laini: Balotelli akivuta sigara kwa hisia kali mjini Miami




Niinue baba: Balotelli akiwa amembeba mpenzi wake baharini

Akiwa mapumzikoni, Balotelli pia aliposti picha akiwa na mkanda wa ubingwa wa dunia wa UFC World katika akaunti yake ya Instagram.
Mtaliano huyo awali alisema kwamba kama asingekuwa mwanasoka, angeibukia kwenye mchezo wa sanaa za mapigano.
Balotelli anafikiriwa yuko njiani kuondoka Milan, ambako alitua miezi 18 iliyopita akitokea Manchester City.


Balotelli akiwa na mkanda wa ubingwa wa UFC




Balotelli akiwa na mashabiki wake katika ufukwe mjini in Florida

Milan iko tayari kumuuza mshambuliaji huyo ili kupunguza bajeti yao ya mishahara, huku Arsenal ikiwa miongoni mwa klabu zinazomtaka.
Balotelli anataka kurudi Ligi Kuu ya England, lakini kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amekanusha kuwa na mpango wa kumsaini mshambuliaji huyo.

Post a Comment

0 Comments