Header Ads Widget

Kocha Gamondi kumuingiza Hafiz Konkoni Kikosi Cha Kwanza

Kocha Gamondi kumuingiza Hafiz Konkoni Kikosi Cha KwanzaMghana, Hafiz Konkoni.

KOCHA Mkuu wa Yanga, Muargentina, Miguel Gamondi, anafikiria kumuanzisha mshambuliaji wake, Mghana, Hafiz Konkoni katika kikosi cha kwanza.

Uamuzi huo umekuja mara baada ya kulikosa kombe la kwanza la Ngao ya Jamii wakitoka kufungwa dhidi ya Simba katika mchezo wa Fainali uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, juzi Jumapili ambao Yanga walifungwa kwa penalti 3-1 baada ya kutoka suluhu dakika 90.

Mshambuliaji huyo ametoka kutambulishwa hivi karibuni na Yanga ambaye amekuja kuchukua nafasi ya Mkongomani, Fiston Mayele aliyeuzwa Pyramids FC ya Misri.

Mghana huyo hadi hivi sasa amecheza mchezo mmoja wa mashindano ukiwa ni ule wa Fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba akitokea benchi kuchukua nafasi ya Clement Mzize.
Kocha Gamondi kumuingiza Hafiz Konkoni Kikosi Cha Kwanza

Akizungumza na Spoti Xtra, Gamondi alisema baada ya kumtumia Konkoni katika mchezo wa fainali, amepanga kuendelea kumtumia mshambuliaji kwenye michezo ijayo.

Gamondi alisema alichopanga hivi sasa ni kuendelea kumuongezea mbinu za kiufundi mshambuliaji huyo, huku akimtengenezea muunganiko mshambuliaji huyo ili awe tegemeo.

Aliongeza kwamba, ilikuwa ngumu kumuanzisha moja kwa moja katika kikosi cha kwanza kilichocheza Ngao ya Jamii kutokana na kuchelewa kujiunga na kambi ya timu hiyo.
“Nimepanga kuanza kumtumia Konkoni kwa kumuanzisha katika kikosi changu cha kwanza katika michezo ijayo ya msimu huu ni baada ya kuona uhitaji wake katika timu.

“Konkoni ni mchezaji mzuri mwenye kiwango bora cha kufunga mabao, na kikubwa kilichosababisha nisimuanzishe kikosi cha kwanza katika Ngao ya Jamii ni kuchelewa kujiunga na timu kambini ambaye usajili wake ulichelewa.

“Nimeona upungufu katika safu yangu ya ushambuliaji ambayo ni lazima nimtumie mshambuliaji halisi mwenye uzoefu na uwezo mkubwa wa kufunga mabao kama huyo Konkoni ambaye ninaamini ataonyesha kiwango kikubwa,” alisema Gamondi

Post a Comment

0 Comments