Nguo zikiwa zimeanikwa baada ya wakazi wa eneo hili kurudi kwenye nyumba zao.
Nguo na magodoro yakiwa yameanikwa.
Magodoro yaliyolowa maji yakiwa yameanikwa.
Familia ambayo haikufahamika mara moja ikifua na kuanika nguo zao.
Maji bado yapo lakini wamehamia hivyo hivyo.
Ikiwa zimepita siku zisizozidi 14 tangu wakazi wa bonde la Msimbazi na Kigogo jijini Dar es salaam kukumbwa na mafuriko na kupelekea wakazi hao kuyakimbia maeneo yao, kamera yetu imeshuhudia wakazi hao wakirejea baada ya mafuriko kupungua.
Mwandishi wetu ameshuhudia wakazi hao wakianika nguo na magodoro yao yaliyoloa maji, pamoja na kupanga vitu vyao, licha ya mvua zinazoendelea kunyesha jijini humo
Ikumbukwe kuwa hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq alikaririwa na vyombo vya habari kuwa wanaoishi mabondeni waondoke mara moja lakini wakazi hao waligoma kuondoka kwa madai kuwa hawana mahali pengine pa kuishi
Mvua bado zinaendelea kunyesha licha ya wakazi hawa kurejea eneo hili ambalo lilikumbwa na mafuriko pia.
Habari/Picha na Eddy Blog
0 Comments