Header Ads Widget

Gavana wa Benki ya Ghana atakiwa kujiuzulu

Gavana wa Benki ya Ghana atakiwa kujiuzulu
Kutoka Nchini Ghana Chama kikuu cha upinzani nchini, kimetoa wiki tatu kwa gavana wa benki na naibu wake kujiuuzulu.

The National Democratic Congress kinamtuhumu Ernest Addison mkuu wa benki hiyo kwa uongozi mbaya, benki hiyo ikikashifiwa kwa kuchapisha pesa kinyume na sheria pamoja na kutumia zaidi ya dolla milioni 8.6 kwa gharama za usafiri.

Ripoti ya hivi punde ya kila mwaka ya benki kuu imeonyesha kwamba ilisajili hasara ya dolla bilioni 5.4 mwaka uliopita.

Benki hiyo tayari imekana tuhumu za chama hicho cha upinzani na kuhusisha hasara hiyo na mpango wa kufanya upya ulipaji wa deni lake kwa mujibu wa makubaliano kati yake na shirika la fedha duniani.

Ghana kwa sasa inajaribu kujiondoa kutoka katika mzozo mbaya zaidi wa kiuchumi. Mnamo Mei nchi hiyo ilipata mkopo wa $3bn kutoka kwa IMF kushughulikia mzozo wa kiuchumi.

Post a Comment

0 Comments