Header Ads Widget

Sudan yateua waziri mpya wa mambo ya ndani

Sudan yateua waziri mpya wa mambo ya ndani

Mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Sudan, Jenerali Abdel Fattah Al-Burhan amemteua mkuu wa jeshil la polisi, Khaled Hassan Mouheiddine kuwa waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo.
Taarifa ya Baraza Kuu la Kijeshi la Sudan imesema: “Al-Burhan amemkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Vikosi vya Polisi, Khaled Hassan, kazi na jukumu la Waziri wa Mambo ya Ndani.”
Hatua hiyo ya Al-Burhan imekuja baada ya kumfuta kazi waziri wa mambo ya ndani aliyepita Anan Hamed Mohammed Omar, ambaye pia alikuwa mkurugenzi mkuu wa polisi.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Sudan, Jenerali Abdel Fattah Al-Burhan kuunda kamati ya kuchunguza uhalifu wa kivita, ukiukaji wa haki za binadamu na uhalifu mwingine ambao anasema unafanywa na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) nchini humo.

Taarifa ya ofisi ya Jenerali Al-Burhan imesema, kamati hiyo ina wawakilishi kutoka ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Sheria, Jeshi, Polisi, Idara ya Ujasusi na Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu.

Sudan imekuwa kwenye mapigano makali ya ndani kati ya jeshi la nchi hiyo na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) mjini Khartoum na maeneo mengine ya Sudan tangu Aprili 15, na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 3,000 na kujeruhiwa zaidi ya 6,000 wengine. Hiyo ni kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya ya Sudan.

Zaidi ya watu milioni 3 wamelazimika kuhama makazi yao, ndani na nje ya nchi, tangu mzozo huo ulipozuka nchini Sudan katikati ya mwezi Aprili mwaka huu. Hayo ni kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa.

Post a Comment

0 Comments