Header Ads Widget

China yaunga mkono mazungumzo ya amani ya Ukraine

China yaunga mkono mazungumzo ya amani ya Ukraine baada ya Saudi Arabia

Waangalizi wamesema Jumapili kwamba Saudi Arabia itakuwa mwenyeji wa mkutano unaolenga kutatua mzozo wa Ukraine kwa amani kunaashiria kuendelea kuimarika kwa ushawishi wa taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta kwenye jukwaa la kimataifa.

Taifa hilo limeleta pamoja takriban mataifa 40 yenye misimamo tofauti yakiwemo Marekani, China na India pamoja na mengine kutoka upande wa kusini, ili kujadili mzozo huo.

Katika siku ya pili ya kikao hicho mjini Jeddah, mazungumzo yalikuwa yakiendelea baina ya mataifa hayo wakati maafisa wakuu kutoka Ukraine pamoja na washirika wake kutoka magharibi kama vile Marekani na Umoja wa Ulaya wakihudhuria, na pia mataifa kutoka upande ya Kusini mwa ulimwengu, ambayo baadhi yamekuwa hayaegemei upande wowote au baadhi yakiwa washirika wa Russia kwenye mzozo huo.

China yaunga mkono mazungumzo ya amani ya Ukraine baada ya Saudi Arabia
China inasemekana kuunga mkono duru ya tatu ya mazungumzo ya kutafuta muafaka wa amani nchini Ukraine baada ya mkutano wa maafisa wakuu kutoka takriban nchi 40 nchini Saudi Arabia mwishoni mwa juma.

Mkutano wa kilele wa siku mbili huko Jeddah ulikuwa wa pili wa aina yake, baada ya kongamano kama hilo huko Copenhagen mapema msimu huu wa joto, na unalenga kuandaa kanuni muhimu za jinsi ya kumaliza vita vya Urusi nchini Ukraine.
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy, alisema anatumai mpango huo ungesababisha “mkutano wa kilele wa amani” wa viongozi wa dunia msimu huu wa vuli ili kuidhinisha kanuni hizo, kwa kuzingatia kanuni zake 10 za suluhu.
China yaunga mkono mazungumzo ya amani ya Ukraine baada ya Saudi Arabia
Mazungumzo hayo ambayo yaliiondoa Urusi, yalihudhuriwa na Marekani, India, EU na mjumbe maalum wa China katika masuala ya Eurasia, Li Hui.

Hii ni mara ya kwanza kwa China kushiriki mazungumzo ya aina hiyo, ingawa Beijing imedumisha ushirikiano wa karibu wa kiuchumi na kidiplomasia na Russia, na kukataa kukemea Moscow wazi wazi kutokana na uvamizi wake.

Hata hivyo Russia haijahudhiria kikao hicho lakini inasemekana kufuatilia kwa kina mazungumzo yanayoendelea.

Waangalizi pamoja na maafisa wa magharibi wanasema kwamba Saudi Arabia imekuwa muhimu katika kushawishi China kuhudhuria mazungumzo hayo.

Maafisa wa Saudi Arabia wanayaona mazungumzo hayo kama hatua muhimu katika kuimarisha sera ya ushirikiano dhabiti na Ukraine, China na Russia.

Post a Comment

0 Comments