kutoka kwa mtu wangu wa nguvu tza millardayo na share na wewe mdau uliyekosa matokeo ya mchezo kati ya yanga na azam, full time ipo hapa.
October 17 ndio siku ambayo Ligi Kuu soka Tanzania bara iliendelea kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja tofauti tofauti, uwanja wa Taifa Dar Es Salaam ulipigwa mchezo ambao uliamua nani atapata nafasi ya kuongoza katika msimamo wa Ligi Kuu soka Tanzania bara.
Kikosi cha Yanga kilichoanza
Dar Es Salaam Young African walicheza dhidi ya Azam FC, mechi hii ilikuwa ni moja kati ya mechi za kuvutia, kwani Yanga na Azam FC zote zina point 15 kila mmoja na wote wamecheza jumla ya mechi 5 ila hii ilikuwa ni mechi ya sita kwa timu zote mbili. Kabla ya mechi kumalizika Yanga alikuwa anaongoza msimamo wa Ligi kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa, lakini mechi imemalizika kwa sare ya goli 1-1.
Kikosi cha Azam FC kilichoanza
Kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika dakika ya 45 Donald Ngoma alipachika goli la kwanza baada ya kuitumia pasi safi kutoka kwa Juma Abdul, kipindi cha pili Azam FC walifanya mabadiliko kwa kumtoa Alan Wanga na kumuingiza Kipre Tchetche mshambuliaji ambaye alitumia vizuri pasi ya Farid Musa dakika ya 83 na kusawazisha goli. Licha ya Yanga kupata penati walishindwa kuitumia baada ya Kamusoko kupeleka mikononi mwa Aishi Manula,
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu October 17
Maji Maji 1 – 0 African Sports
Mbeya City 0 – 1 Simba
Ndanda FC 0 – 0 Toto African
Stand United 3 – 0 Tanzania Prisons
Coastal Union 0 – 1 Mtibwa Sugar
Alan Wanga akijaribu kumtoka Haji Mwinyi wa Yanga
Mbuyu Twite wa Yanga akidhibitiwa na Agrey Morris
Alan Wanga akidhibitiwa na Nadir Haroub
Kocha msaidizi wa Azam FC Mario Marinca akimpa maelekezo John Bocco
Shomari Kapombe na Haji Mwinyi wakiwania mpira
Mbuyu Twite akimdhibiti Himid Mao asipite kuelekea langoni kwao
Mashabiki wa Yanga baada ya timu yao kupata goli la kuongoza
Msuva na Juma Abdul wakijaribu kumkaba kwa pamoja Farid Musa
John Bocco akiwa katika harakati za kutafuta goli la kusawazisha
Wachezaji wa Azam FC wakishangilia goli la Tchetche baada ya kusawazisha.
Wachezaji wa Azam FC wakishangilia goli la Tchetche baada ya kusawazisha.
Simon Msuva akipatiwa matibabu baada ya kufanyiwa faulo ndani ya uwanja
Donald Ngoma akishangilia baada ya kufunga goli
0 Comments