Header Ads Widget

MPYA: WASHUKIWA WAWILI WAKAMATWA KWA KULIPUA BOMU MGAHAWANI ARUSHA


Watu wawili wamekamatwa na Polisi wakihusishwa na shambulio la bomu lililotokea kwenye mgahawa wa 'Vama Traditional Indian cuisine' jijini Arusha.


Shambulizi hilo liliyokea Jana siku ya jumatatu saa nne usiku.



Watu wasiojulikana walirusha bomu ndani ya mgahawa kupitia mlangoni ambapo watu wanane wamejeruhiwa moja kati yao akiwa na majeraha makubwa.


Aidha,katika matukio mengine, jumla ya Watu 20 wanazuiliwa na Polisi wakiwemo watu sita wanaosadikiwa kujihusisha na mlipuko wa bomu uliotokea mkoani Arusha juma lililopita nyumbani kwa Kiongozi wa dini Sheikh Sudi Ally Sudi na kujeruhi watu wawili.


Polisi wanaendelea na upelelezi kuhakikisha inawatia nguvuni watu waliohusika na matukio hayo.


Haijulikani kilichosababisha mlipuko huo.

Post a Comment

0 Comments