
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa George Tyson kuupeleka mochwari.

Jeneza lenye mwili wa George Tyson likiingizwa mochwari katika Hospitali ya Kairuki, Mikocheni jijini Dar.

Dada wa marehemu Tyson, Doreen akilia kwa simanzi baada ya mwili wa kaka yake kuwasili.

Doreen akiwa amepoteza fahamu baada ya mwili wa kaka yake kuwasili Hospitali ya Kairuki.

Mwili wa Tyson ukiwa mochwari katika Hospitali ya Kairuki.

Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve Nyerere, akiwasili katika Hospitali ya Kairuki kusubiri mwili wa marehemu. Steve alivalia tisheti yenye ujumbe 'Why always me'.

Gari lililobeba mwili wa marehemu Tyson, aina ya Toyota Land cruiser lenye namba za usajili STK 6630 kutoka Wilaya ya Mvomero likiwasili Hospitali ya Kairuki kutoka mkoani Morogoro.

Gari hilo baada ya kuwasili na mwili wa Tyson.

Msanii wa filamu za Kibongo, Kelvin akihojiwa kuhusu alivyopokea taarifa za kifo cha mwongozaji filamu, George Tyson.

Mr. Chuz akielezea alivyoupokea msiba wa George Tyson.

Wema Sepetu akihojiwa na mwanahabari wakati wa kupokea mwili wa Tyson.

Mwigizaji Aunt Ezekiel naye alikuwepo kupokea mwili wa Tyson.

Mastaa wa filamu, Rose Ndauka (kushoto) na Jack Pentzel wakiwa Hospitali ya Kairuki kuupokea mwili wa Tyson.

Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve Nyerere akibadilishana mawazo na mmoja wa waombolezaji.
PICHA NA GPL
0 Comments