Header Ads Widget

Allan Okello awaaga rasmi Vipers, kushuhudia Azam FC vs Yanga

Allan Okello awaaga rasmi Vipers, kushuhudia Azam FC vs Yanga

WINGA mpya wa Yanga SC, Allan Okelo amewaaga rasmi wachezaji wa timu ya Vipers United na benchi la ufundi.
Nyota huyo ametambulishwa rasmi kuwa ni njano na kijani usiku wa kuamkia leo Januari 13 2026 ikiwa ni zawadi ya Mapinduzi.
Okelo raia wa Uganda ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa AFCON 2025 nchini Morocco na kikosi cha timu ya Taifa ya Uganda kilichoishia hatua ya makundi.
Alianza kikosi cha kwanza kwenye mchezo dhidi ya Tanzania uliokamilika kwa wababe hawa kutoka Afrika Mashariki kugawana pointi mojamoja kwa kufungana goli 1-1.
Akiwaaga wachezaji na benchi la ufundi amebainisha kwamba anawaombea kila la kheri kwenye kutimiza majukumu yao ya kila siku.
“Imekuwa ni muda mzuri kwangu kwa miaka miwili niliyokuwa hapa, wakati mwingine kwa ajili ya changamoto mpya umefika hivyo ninawaombea kila la kheri,”.

Okelo atashuhudia fainali ya NMB Mapinduzi Cup Azam FC vs Yanga SC leo unaochezwa Uwanja wa Gombani, Zanzibar.
.

Post a Comment

0 Comments