Umoja wa wana Kukaya Miono wilaya ya chalinze mkoani pwani, baada
ya kuhitimisha mjadala wa elimu waliingia katika utekelezaji na hatua iliofuata
ilikuwa ni kuchimba msingi wa chumba cha darasa shule ya msingi miono, zoezi ambalo liliisha vizuri na baada ya hapo wakapanga
siku maalum kwaajili ya kuzindua ujenzi wa darasa hili.
Zoezi hili la uzinduzi lilihudhuriwa
na wadau mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali na lengo likiwa ni kuweka jiwe la
msingi, kutangaza malengo ya group la kukuya Miono na pia kutangaza harambee ya kuchangisha michango
kwa wote watakaoguswa kwa namna moja ama nyingine kuungana na jitihada za wana
kukaya Miono.
Hafla hio ilipangwa na viongozi
wa group hilo akiwemo kiongozi mkuu na mwanzilishi wa group hili bwana Omari
Mtiga na viongozi wengine wa group kama vile ndugu Sadiki Mchama, Juma Salum na
wajumbe wengine.
Mgeni Rasmi.
Mgeni rasmi wa shughuli
alikuwa Mkurugenzi wa taasisi ya TETE Foundation Bi. Susan Senso ndie aliyeweka Jiwe
la msingi akitangulizana na viongozi mbalimbali
Mbali na mgeni rasmi wengine waliokuja kuwaunga mkono wana kukaya Miono ni umoja wa Kibindu Tunayoitaka ambao waliahidi kuchangia tofali 100 na kusema pia zinaweza zikazidi. Wengine pia walikuwa kutoka katika Kijiji cha Mkange ambao nao walihudhuria uzinduzi huu.
Tazama video ya wana kibindu wakiahidi kuchangia
Kwa ujumla kila kitu kilienda vizuri hapa chini ni baadhi ya picha kutoka eneo la tukio shule msingi Miono ambako uzinduzi ulifanyika.
0 Comments