Header Ads Widget

Wanachi wajitokeza kuchimba msingi wa chumba cha darasa shule ya msingi miono

Wananchi waungana na Kukaya Miono Katika Uchimbaji wa Msingi wa darasa

Historia kwa ufupi

Baada ya kuanzishwa kwa umoja wa Kukaya Miono Mnamo tarehe 6 mwezi 12 mwaka 2023, Mada iliojadiliwa ilikuwa kuhusu elimu na mwisho ikahitimishwa kwa kukubaliana kuanza kujenge chumba cha darasa tukianza na shule ya msingi ya Miono japo changamoto upande wa elimu zilikuwa ni nyingi lakini iliopewa kupaumbele ni ujenzi wa darasa. Kujua malengo ya Group hili Bofya hapa kusoma

Utekelezaji wa uchimbaji

Siku kadhaa baadae ikapangwa siku ya kukutana wana umoja wote wa Kukaya Miono na kuhamisisha na wananchi pia kwaajili ya zoezi la kuanza kuchimba msingi wa chumba hicho cha darasa. Kwenye mada hii umoja ulikubaliana kuwa hawawezi kununua kwa kila kitu vitu vingine lazima vitafanywa na wao wenyewe.

Wengi walivutiwa na umoja huu wananchi wengi walishiriki katika zoezi hili na lilienda vizuri, walihudhuria watu mashughuli kutoka kijijini hapo akiwemo Mheshimiwa Diwani Juma Mpwimbwi, Mwana Miono ambae anatokea Canada na jumuiya ya wazazi wa CCM Miono nao pia walihudhuria.

Tazama baadhi ya picha mbalimbali zikionyesha zoezi likiwa linaendelea
Wananchi waungana na Kukaya Miono Katika Uchimbaji wa Msingi wa darasa
Wanachi wajitokeza kuchimba msingi wa chumba cha darasa shule ya msingi miono


Post a Comment

0 Comments