Header Ads Widget

Kibindu Tunayoitaka Waanza Kutekeleza Ahadi Yao kwa vitendo ujenzi wa darasa Miono.

Kibindu Tunayoitaka Waanza Kutekeleza Ahadi Yao kwa vitendo.
Mwenye Tshirt ya Blue bahari ni Mwakirishi wa wana Kibindu tunayoitaka

Siku ya Jumamosi tarehe 10 Feb, 2024 ilikuwa ni Siku ya uzinduzi wa Ujenzi wachumba cha darasa shule ya msingi Miono wilaya ya Chalinze, Mkoani Pwani, wageni waalikwa ambao nao ni wana umoja unajulikana kama Kibindu tunayoitaka siku hio waliahidi kuchangia tofali 100 na kusema kuwa yanaweza yakazidi. Leo tare 12 feb, 2024 wameeanza kutekeleza ahadi yao kwa vitendo kwa kuanza kuchangisha fedha wao kama wao kwaajili ya kununua tofali 100 na mpaka jioni hii wamekusanya kiasi cha shilingi 143,000/= na michango bado inaendelea.

Kama hukuiona video ya wana Kibindu wakiahidi kuchangia tofali 100 bonyeza play kuitazama, 

pia kuona video mbalimbali kutoka katika tukio hilo ingia youtube channel ya Miono TV, Au bofya hapa kutazama video

Kibindu Tunayoitaka Waanza Kutekeleza Ahadi Yao kwa vitendo ujenzi wa darasa Miono.


Post a Comment

0 Comments