Header Ads Widget

Wana Miono Waunda Group la Maendeleo “Kukaya Miono"

Wana Miono Waunda Group la Maendeleo “Kukaya Miono"

Kutoka Chalinze Mkoani pwani katika Kijiji cha Miono, Wana Miono wazawa waishio Miono, nje ya Miono na hata nje ya nchi ya Tanzania lakini ni ni wazaliwa wa Miono, wameamua kuanzisha Group la WhatsApp linalojulikana kama “Kukaya Miono” Neno la Kizigua lenye maana ya “Nymbani Miono”

Lengo La Group hili

Lengo kuu la kuundwa kwa group hili ni kuchangia maendeleo ya Miono hasa katika kufuatilia miradi ya maendeleo ya serikali kujua changamoto na kutafuta suruhu ili kuhakikisha maendeleo yanakuja Katika Kijiji chao, Hio kwa jumla

hapa chini nakushirikisha malengo na kanuni za group hili kama ifuatavyo.
  1. Umoja wa Wana Miono - Wazawa, Wanaoishi nje na ndani ya Miono na Wadau wa Miono
  2. ⁠Kufahamishana juu ya yanayojiri Miono na kuhusiana na Wana Miono
  3. Dhamira Kuu ni kuleta na kushawishi maendeleo na tija kwenye jamii yetu ya Miono
  4. Umoja huu unadhamiria kuleta mchango chanya Miono kwenye Sekta mbalimbali - Hasa Elimu, Afya, Kilimo, Sanaa na Michezo
  5. Umoja unadhamiria kuleta na kushawishi maendeleo kwenye jamii ya Miono kupitia kushirikisha nguvu za Wananchi (Wa ndani na nje ya Miono), Viongozii., Taasisi mbalimbali nk
  6. Umoja huu haufungamani na Dini, Kabila wala Siasa za namna yoyote bali utashirikiana na Viongozi wa namna zote katika kufanikisha tija kwenye jamii yetu ya Miono ••Matumizi ya lugha ya Kizigua kwenye Group la Kukaya Miono hayakatazwi
  7. Umoja huu wa Kukaya Miono unadhamiria kuchangia kwa kadrii inavyowezekana kusafirisha misiba ya Wana Miono iliyotokea nje ya Miono ila wanakwenda kuzikwa Miono. Kwa kila msiba unaotokea taarifa zitaletwa kwenye Group na michango kupitishwa (Kila mwanachama kiwango chochote kile)
  8. Umoja unaweka nia ya kuleta utamaduni wa Wana Miono kutenga muda maalum wa Ziara kila mwaka kwenda Miono kutembelea miradi na harakati mbalimbali za maendeleo kwa lengo la kuleta na kushawishi maendeleo. Pendekezo la awali ni kutumia Siku ya Mahafali Kikaro Sekondari kama kilele cha Ziara hiyo
  9. Kwenye Group la Kukaya Miono hakuruhusiwi kutumwa jambo lolote lenye maudhui ya matusi, kashfa, siasa, dini. Group linakataza pia mambo ya michezo (Simba na Yanga) isipokuwa taarifa za michezo ya Miono au Wana Miono. Group halikatazi kutumwa taarifa za kitaifa/kimataifa au za ujumla (General news/Information)
  10. Umoja utaratibiwa na Uongozi (Admins) utakaosimamia maudhui yanayotumwa kwenye Group na kuchukua hatua pale kanuni zinapokiukwa - mfano kumuonya au kumtoa mwanachama kwenye Group
  11. Kanuni na Malengo ya sasa yataendelea kuhuishwa na kuboreshwa kadri inavyohitajika

Admins

16/12/2023

Post a Comment

0 Comments