Mtoto Wa Rais Gustavo Petro Wa Colombia Akamatwa Kwa Utakatishaji Fedha
Mtoto wa Rais Gustavo Petro wa Colombia amekamatwa kwa utakatishaji fedha na utajiri haramu.
Nicolas Petro, ambaye pia ni Mwanasiasa alikamatwa kwa tuhuma za kupewa pesa na wasafirishaji wa dawa za kulevya akidai zitafadhili kampeni za uchaguzi zilizokuwa zikifanywa na baba yake.
Katika tuhuma hizo, aliyekuwa mke wa Nicolas, Bi. Daysuris del Carmen Vasquez naye amekamatwa.
Bi. Vasquez aliwahi kuviambia vyombo vya habari kuwa mnamo mwaka jana mume wake wa zamani alitumia jina la baba yake kupata takribani pauni 120,000.
Mwanamama huyo alieleza kuwa alikuwepo wakati wa mikutano kati ya Nicolas na wadau wa dawa za kulevya na kuwa pesa alizopewa walikwenda kuzihifadhi nyumbani kwao.
Nicolas, amekana mashtaka huku baba yake ambaye ni Rais Petro akikana kupokea pesa zilizotoka kwa wadau wa dawa za kulevya.
Rais huyo amewaamuru waendesha mashtaka kumchunguza mtoto wake na ameahidi kutotumia nafasi yake kuingilia uchunguzi huo kwa namna yoyote.

Kupitia mtandao wa X, Rais huyo ameandika ”Inaumiza kwa mmoja wa watoto wangu kukamatwa na kuwekwa rumande, lakini sitoingilia uchunguzi”
“Kijana wangu ninakuombea kheri na nguvu, naomba matukio haya yakubadilishe na upate muda wa kuyatafakari makosa yako”.
0 Comments