Jumla ya wanafunzi 111 wamepata mimba kwa kipindi cha mwaka 2012/13 katika shule za msingi na sekondari mkoani Lindi na 1405 kati ya 8399 waliochaguliwa kujiunga elimu ya sekondari mwaka huu mkaoni Lindi hawajafika kwenye shule hizo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utoro,
Hayo yamebainishwa na afisa elimu mkoa Silas Semaluku alipokuwa anazungumza na wadau wa elimu kwenye mkutano wa wadau wa Elimu mkoani Lindi.
Semaluku alisema mkoa una kabiliwa na changamoto kubwa za watoto kupata mimba kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo tamaa kwa watoto wakike kuwa na vitu vya thamani ambazo zimeanza kufanyiwa kazi , na idara ya elimu pamoja na wazazi,
Alisema wilaya Lindi inaongoza kwa kuwa na watoto wengi waliopata ujauzito ambao 48 ikifuatia wilaya Kilwa 23, Nachingwea 18, Ruangwa 14, Liwale 6 na manispaa ya Lindi 2.
Semaluku alisema kuwa mkoa ulipangiwa wanafunzi 8,399 kati yao wasichana 4,078 na wavulana 4,321 lakini waliofika shuleni hadi sasa ni 6,994 pia wanafunzi 1,405 hawajafika shule hadi sasa kati yao wavulana 720 na wasichana 685.
Alifanunua kuwa wanafunzi halmashauri ya wilaya Lindi kuna wanafunzi 327 wahajafiki shule hadi sasa, Liwale wanafunzi 230, Kilwa 200 Ruangwa 351 wilaya ya Nachingwea 226 huku Manispaa ya Lindi ikiwa na wanafunzi 69.
0 Comments