Header Ads Widget

Prof. Kitila Mkumbo, "Serikali haiwezi kuuza bandari na bandari haiuziki"

Prof. Kitila Mkumbo, "Serikali haiwezi kuuza bandari na bandari haiuziki"

"Serikali haiwezi kuuza bandari na bandari haiuziki"-Prof. Kitila Mkumbo 

Ni Julai 29, 2023 ambapo Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Daniel Chongolo anazungumza na Wananchi kweny Mkutano wa Chama ulioandaliwa Kawe Jijini Dar es Salaam huku akiongozana na viongozi mbalimbali wa Chama hicho.

Hapa nimekusogezea Nukuu za Prof. Kitila Mkumbo- Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji akizungumzia kuhusu Uwekezaji wa bandari.
‘Serikali haiwezi kuuza bandari na bandari haiuziki, huu ndiyo mkataba pekee tangu nchi hii iundwe wa IGA ambao uko wazi,” Prof. Kitila Mkumbo- Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji.

‘Mheshimiwa Waziri Mkuu alisema Bungeni maoni ya watanzania yamesikilizwa na hofu zao na yatazingatiwa kuhakikisha kwamba yatafanyiwa kazi, na hatuna tatizo kwasababu tunatambua kwamba mkataba huu kama ilivyo mikataba mingine, Serikali haijasaini Bibilia wala haijasaini Quran, imesaini Mkataba mikataba yote duniani uwa inarekebishika na kipo kipengele ambacho kinaruhusu marekebisho ambayo ni ibara 22 ambacho kinaruhusu Marekebisho’- Prof. Kitila Mkumbo- Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji.

‘Kwahiyo Serikali haina tatizo na wataalum, na watanzania wenye nia njema wanaosema uwekezaji uendelee na baadhi ya vipengele vya kwenye mkataba viangaliwe Serikali itafanyia kazi maoni ya Wananchi waliyoyatoa’- Prof. Kitila Mkumbo- Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji.

Post a Comment

0 Comments