Kituo cha Taifa cha Takwimu nchini Uingereza kimetangaza kuwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja tu karibu
watu milioni mbili wamekuwa wahanga wa unyanyasaji wa kingono katika nchi hiyo na kwa muda sasa, ongezeko la visa vya ubakaji na uhalifu dhidi ya wanawake na wasichana nchini Uingereza na kushindwa kushughulikiwa malalamiko yao hususani na polisi kumeibua malalamiko ya ukosoaji na maandamano ya mashirika ya kiraia yanayotetea haki za wanawake nchini humo.
Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB Kituo cha Taifa cha Takwimu cha Uingereza kimeripoti kuwa watu milioni moja na laki tisa nchini humo walikuwa waathirika wa unyanyasaji wa kingono katika kipindi cha mwaka mmoja uliomalizikia Machi 2022.
Kulingana na takwimu za kituo hicho watu milioni moja na laki moja miongoni mwa waathirika hao wa ubakaji ni watu wazima, 798,000 kati yao wakiwa ni wanawake na laki mbili na 57 elfu wanaume.
Kwa mujibu wa ripoti ya
Kituo cha Taifa cha Takwimu cha Uingereza watu milioni saba na laki tisa nchini Uingereza walikuwa walengwa wa unyanyasaji wa kingono au waliandamwa na vitisho vya kudhalilishwa kingono.
Vyombo vya habari vya Uingereza vimeripoti kuwa, baada ya kufichuliwa ripoti za unyanyasaji wa kingono uliofanywa na makumi ya maafisa wa polisi, imani kwa polisi ya nchi hiyo imepungua kwa kiwango kikubwa
0 Comments