Mchungaji wa Malindi Paul Mackenzie, mkewe Rhoda Mumbua Maweu na washukiwa wengine 16 wamewashutumu maafisa wa polisi kwa kuwanyima chakula na kuwapiga wakiwa mahabusu.
Akizungumza na waandishi wa habari katika mahakama ya Shanzu siku ya Ijumaa, Mackenzie ambaye bado hajafunguliwa mashtaka rasmi alibainisha kwamba baadhi ya maafisa ambao wanawashikilia wamekuwa wakiwanyanyasa na kuwaacha njaa tangu walipokamatwa kwa madai dhidi yao.
chakula, ndio, na baadhi yetu hata wamekuwa wakipigwa, ndio,” Mackenzie alilalamika.
“Tumekuwa tukinyimwa Washukiwa walifikishwa mahakamani siku ya Ijumaa huku upande wa mashtaka ukiomba kuwazuilia zaidi ili kukamilisha uchunguzi.
Mawakili wanaowawakilisha washtakiwa, Elisha Komora na George Kariuki waliambia korti kuwa wateja wao walikuwa wakidhulumiwa mahabusu.
“Madai ya Serikali kuwa watuhumiwa waendelee kushikiliwa ili wapate lishe, ni ya upotoshaji, leo asubuhi washukiwa wote hawakupata kifungua kinywa, walinyimwa chakula kwa siku mbili tangu walipotoka mahakamani Mei 2,” alisema Komora.
Paul Mackenzie, ambaye ni kiongozi wa Kanisa la Good News International, anakabiliwa na makosa makubwa ya mauaji, kushauri na kusaidia watu kujiua, utekaji nyara, kuendeleza itikadi kali, mauaji ya halaiki, uhalifu dhidi ya binadamu, ukatili wa watoto, utapeli, ulaghai miongoni mwa mengine.
Ijumaa, timu ya mashtaka inayoshughulikia kesi dhidi yake iliomba mahakama kuruhusu serikali kumzuilia mshukiwa, na washtakiwa wenzake, kwa siku 90 zaidi ili kuruhusu kukamilika kwa uchunguzi.
0 Comments