Mahakama Kuu ya Tanzania imekwama usikilizwaji wa Kesi ya Wabunge wa Viti Maalum 19
Mahakama Kuu ya Tanzania imekwama kuendelea na usikilizwaji wa kesi iliyofunguliwa na Wabunge wa Viti Maalum 19 akiwemo Halima Mdee kutokana na Jaji kutokuwepo.Kesi hiyo nambari 36 ya mwaka 2022 ya kupinga uamuzi wa kuvuliwa uanachama kwa wabunge hao imeahirishwa hadi Mei 2023 ambapo leo iliitishwa kwa ajili ya kusikilizwa.
Kesi hiyo ilitarajiwa kusikilizwa mbele ya Jaji Cyprian Mkeha hata kupitia Ofisi ya Msajili imepanga kuendelea na kesi hiyo hadi Mei 18 na 19, 2023 ambapo leo Halima Mdee na wenzake walipanga kumuhoji maswali ya dodoso mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA, Ruth Mollel.
Mdee na wenzake walifungua kesi hiyo ili kuiomba mahakama ifanye mapitio dhidi ya mchakato uliotumika kuwavua uanachama wa CHADEMA wakidai haukuwa halali kwa madai kuwa hawakupewa nafasi ya kusikilizwa na ulikuwa na upendeleo
0 Comments