Header Ads Widget

BASATA: Hatujaufungia wimbo wa Ney wa Mitego ila haufai kwa jamii



Baada ya rapa Ney wa Mitego kuachia wimbo wake wa Shika adabu yako ambao amewaponda watu kadhaa ikiwemo baraza la sanaa Tanzania kumekwepo na tetesi kuwa wimbo huo umefungia na baraza hilo.

Kwa upande wao BASATA wamesema hawajatoa tamko lolote.Katibu mkuu wa BASATA Godfrey Mngeleza amesema kuwa “naona watu wenyewe wameanza kuufungia,ndio uzuri wa watu wako very effective..hatujatoa tamko hilo lakini tutachukua hatua kutokana na sheria na taratibu,lakini kama watu wameanza kulalamika ujue huo wimbo haufai” alifunguka kiongozi huyo wa BASATA.

Source: Clouds Fm

Post a Comment

0 Comments