Header Ads Widget

Ukaguzi Wa Miradi Ya Maendeleo Kibindu Tunayoitaka (2023)

Ukaguzi Wa Miladi Ya Maendeleo Kibindu Tunayoitaka 2023
Wazigua wa kijiji cha Kibindu waliounda Group La WhatsApp la maendeleo la Kibindu Tunayoitaka wakiwa katika picha ya pamoja wakikagua moja ya mladi wa maendeleo kijijini hapo

Yaliyomo

1. Kuanzishwa WhatsApp Group la Kibindu Tunayoitaka 
2. Lengo La Kundi na Waanzilishi Wake
3. Mafanikio Ya Kundi

Karibu katika blogu hii ya kwetu miono, Leo naenda kukushirikisha habari ambayo naamini itakushangaza Na kukuvutia pia, na hii ni kutoka katika kijiji cha Kibindu kilichopo mkoani pwani njia ya tanga karibu kabisa na mkoa wa tanga, Kijiji ambacho wananchi wake waliamua kujitoa kwa hali na mali ili kuleta maendeleo katika kijiji chao. Wananchi hao waliamua kufanya yafuatayo.

1. Kuanzishwa WhatsApp Group la Kibindu Tunayoitaka
Group hili la WhatsApp lilianzishwa mnamo Mwezi December 2015, Mpaka sasa Group lina wanachama 245 kutoka ndani na nje ya Kibindu na pia nje ya Tanzania.

2. Lengo La Kundi na Waanzilishi Wake
Lengo kubwa la Kundi hili ni Kuleta Maendeleo kwenye kijiji hiki katika sekta mbali mbali hasa Elimu, Ulinzi na Usalama 

Waanzilishi ni Wazawa wa Kibindu waishio nje ya Kibindu ambao Mkomwa Mtiga, Omari Mtiga, Mohammed Amiri Mnangwa, Omari Mbega, Mharami Dipwile, Juma O Almasi, Mwajuma Mchuka

Na hao ndiyo Viongozi (Admins)

3. Mafanikio Ya Kundi

1. Mpaka sasa Group limeshapeleka takribani TZS 50m kwenye maendeleo ya Kibindu kwa michango ya moja kwa moja ya wana group na ya kuhamasishwa na wana Group. Tuna imani kwamba uwekezaji huo umevutia uwekezaji wa zaidi ya TZS 500m Kibindu toka Serikali ya Kijiji, Halmashauri, Serikali Kuu na Taasisi mbalimbali

2. Shule ya Msingi Kibindu
2.1 Ujenzi wa Darasa 1 na Ofisi ya Walimu
2.2 Kupeleka Watoto wa shule kwenye mashindano ya Kimataifa ya Taasisi ya Room to Read
2.3 Kuhamasisha ukuaji wa viwango vya elimu kupitia motisha kwa Walimu na Wanafunzi
2.4 Ujenzi wa Mwalimu House

3. Sekondari 
3.1 Uchangiaji kuvutwa maji shuleni
3.2 Kuanzishwa kwa Kibindu Tunayoitaka Scholarship- kuwazawadia best students

4. Ulinzi na Usalama
Ujenzi wa Kituo cha Polisi Kibindu

5. Kuwaunganisha Wana Kibindu wa kada mbalimbali kushiriki kwenye maendeleo ya Kibindu. Kuna Ziara ya kila mwaka kutembelea miradi ya maendeleo na kufanya mikutano na Viongozi na Wananchi ili kufanikisha vipaumbele

6. Misiba
Group linachangia kila msiba wa Mwana Kibindu unaokwenda kuzikwa KIbindu. Kwa mwaka tunachangja si chini ya misiba 5/6, na kila mmoja wastani wa michango ni TZS 600K/700K

7. Kufanikisha Group kuwa na Identity Yake ndani na nje ya Kibindu. Group lina logo (Nembo) na linachapisha TShirts kila mwaka

8. Kipaumbele 2024
Tumekubaliana kujenga Darasa 1 kwenye shule ya Msingi ya pili (Chapuku)

9. Pia Group limefanikiwa kuanzisha Sub-groups La Michezo na pia la Dini (Kibindu Muslims)

Ukaguzi Wa Miladi Ya Maendeleo Kibindu Tunayoitaka 2023
Picha ya pamoja wana kibindu katika ukaguzi wa miradi 2023

Kibindu Muslims limefanikisha mambo makuu 4

  1. Kusambaza vitabu vya Dini kwenye kila madrassa na msikiti wa Kibindu - thamani takribani TZS 1m
  2. Kuchangia uwekaji wa kipaza sauti kwenye msikiti mkuu Kibindu - takribani Sh 250K
  3. Mwaka huu kuchangia TZS 900K kwenye ujenzi wa msikiti wa Kisatuni (Al Masjid Nuur)
  4. Kuweka awareness ya kila madrassa na msikiti kwa kuweke Walezi ambao ni members wa Group la Muslims
Baadhi ya picha Kutoka Kibindu Tunayotaka wakikagua miradi yao mwaka huu 2023
Ukaguzi Wa Miradi Ya Maendeleo Kibindu Tunayoitaka (2023)
Ukaguzi Wa Miradi Ya Maendeleo Kibindu Tunayoitaka (2023)

Ukaguzi Wa Miradi Ya Maendeleo Kibindu Tunayoitaka (2023)
Ukaguzi Wa Miradi Ya Maendeleo Kibindu Tunayoitaka (2023)

Ukaguzi Wa Miradi Ya Maendeleo Kibindu Tunayoitaka (2023)
Mwana Miono Sadiki Juma Mchama Akijumuika na wana Kibindu Tunayoitaka

Ukaguzi Wa Miradi Ya Maendeleo Kibindu Tunayoitaka (2023)
Tshirts Za Kibindu Yunayoitaka zenye ujumbe wa lugha ya kizigua
yenye maana kwamba "Tumekutana Kibindu, Nyumbani Raha, Wote ni sisi"


Hayo ndio niliokushirikisha leo kutoka katika kijiji cha kibindu bila shaka umejifunza mengi na naamini huenda ukapata wazo la kuanzisha hili katika kijiji chako sio mbaya kuiga mambo ya maendeleo kama hujui wana Miono Nao wako mbioni kuipambania miono yao. kama una maoni usisahau kutuachia hapo kwenye comment box

Post a Comment

0 Comments