Uongozi wa kizazi kipya upo tayari kushika hatamu za uongozi na kuijenga Tanzania mpya, kwa fikra mpya na maarifa mapya. Mabadiliko, kokote yalikotokea, yalidaiwa na kuongozwa na vijana. Vijana wa Tanzania washike usukani wa kuleta mabadiliko wanayoyataka. Ukiona kijana anamwambia kijana mwenzake hana uzoefu, basi kazi ya kuleta mabadiliko ni kubwa zaidi. Kutokuwa na uzoefu ni sifa ya kijana. Tusi kubwa kwa Obama mwaka 2008 lilikuwa ni kukosa uzoefu, kukosa rekodi. Tusi hilo lilikuwa muziki kwa wapiga kura wa Marekani. Tanzania mpya inahitaji viongozi wapya, mazoea mapya, fikra mpya na maarifa mapya. Inahitaji kuthubutu mambo makubwa sio kulinda uzoefu wa nyuma. Tunaweza.
source .January Makamba
0 Comments