HEE! Baba mchungaji, ni nini hiyo? Ndivyo walivyosikika wakiuliza baadhi ya watu waliokatiza kwa Mchungaji Michael Semeni wa Kanisa la Living Word Ministry lililopo Ukonga- Majumba Sita jijini Dar es Salaam.
Mkasa mzima ulijiri Julai 3, 2014 ndani ya ofisi za mchungaji huyo huku mlalamikaji mkuu akiwa na mwanaume aliyedaiwa kuwa ni mume wa mwanamke aliyekutwa na Semeni.
Sekeseke hilo lilitokana na madai kwamba, Mchungaji Semeni alinaswa akiwa na mwanamke huyo aitwaye Erizabert Kisanda, mkazi wa jijini Mwanza ambaye alifika Dar kuonana naye kwa ajili ya kumwombea maombi maalum ya kiroho ‘deliverance’ kutokana na matatizo ya mke huyo kushika mimba na kutoka kila wakati.
OFM KAMA KAWAIDA YAKE
Siku ya tukio, makamanda wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) walikuwa mitaani katika viunga mbalimbali vya Jiji la Dar wakisaka matukio, ndipo walipojikuta wakitokea eneo lenye kimbembe.
Baadhi ya watu waliozungumza na Ijumaa Wikienda walidai kuwa mchungaji huyo alinaswa na mke huyo wa mtu hivyo kuzua tafrani kati yake na mwanaume anayedaiwa ni mumewe.
Mchungaji akihojiwa na kamanda aliyeshirikiana na OFM katika operesheni hiyo ya kufichua uovu kanisani hapo.
MTU WA KARIBU
Akizungumza na gezeti katika eneo la tukio, mtu mmoja aliyedai ni ndugu wa mwanamke huyo alisema:
“Iko hivi! Huyu mwanamke alikuja Dar kwa mchungaji kwa lengo la kuombewa apate mtoto. Alikuwa na tatizo la uzazi kwani kila alipopata ujauzito, akikaribia kujifungua tu mimba inaharibika.
“Kutokana na tatizo hilo, ndipo akashauriwa akamwone mchungaji huyo ndipo akafunga safari kwenda kumuona na kumweleza tatizo lake, mchungaji akamwambia ni tatizo dogo sana kwake.”
AHADI YAPANGWA
Ilizidi kudaiwa na ndugu huyo kwamba, ahadi ilipangwa ambapo mwanamke huyo alitakiwa kurudi siku hiyo ya tukio.
Mchungaji akichukuliwa kwenda polisi. MAOMBI YALIVYOKUWA
Mambo yaliendelea kuhabarisha kwamba, siku ya tukio, mwanamke huyo alifika kuombewa ambapo mchungaji huyo alizama kiroho zaidi kwa muda wa saa mbili, yaani dakika mia na ishirini.
“Baada ya kumaliza maombi hayo ndani ya kanisa ndipo mchungaji huyo akamchombeza kwa kumwambia wazame chumbani akamwombee zaidi,” chanzo kilisema.
AKUTWA NA PENSI!
Wapashaji wa mkasa huu wanadai kuwa wakiwa chumbani sasa, mke hana nguo, mchungaji akiwa ndani ya kipensi tu, mwanaume aliyedaiwa ni mume na dada yake walitokea kusikojulikana na kuwavaa.
Huu ni mwonekano wa ndani wa kanisa la Living Word Ministry lililopo Ukonga, Majumba Sita jijini Dar es Salaam. NENO SAMAHANI
Baada ya kunaswa, mchungaji huyo alirudiwa na fahamu na kuanza kuomba asamehewe huku akimlaumu shetani kwamba alimpitia naye akapitika kweli.
“Duh! Yamenikuta jamani, naomba mnisamehe ni shetani tu alinipitia,” alisikika akisema mchungaji huyo.
MUME ALIJUA?
Swali kubwa lililotawala eneo la tukio ni kuibuka kwa mwanaume huyo, kwamba alijua mkewe anakwenda kwa mchungaji huyo?
Baadhi ya watu walisikika wakisema kuwa wana wasiwasi kwamba, mwanaume huyo, mkewe na mawifi walijua litakalokwenda kutokea kwa mtumishi huyo wa Mungu hivyo walimtega naye akauingia mtego huo!
Bango linaloonyenesha ratiba za ibada zinazofanyika kanisani hapo
ALICHOMWA?
Maneno ya watu ni mengi sana, mawifi nao walisikika wakimsakama mchungaji kwa kudai kuwa alizoea kuchezea wengine lakini si kwa wifi yao huyo bila kufafanua maana ya madai yao hayo hivyo kujenga dhana kwamba huenda kuna watu walimchoma mchungaji huyo kwa mume wa mwanamke huyo.
NI KWELI MIMBA HUHARIBIKA?
Baada ya kumalizika kwa tafrani hiyo, OFM walipenda kujua kama madai ya mwanamke huyo kuharibu mimba kila anapokaribia kujifungua ni ya kweli, wifi mmoja alithibitisha ni kweli na kwamba, mwanamke huyo ameshazunguka sana kutafuta dawa ya kuondoa tatizo hilo lakini wapi!
MALALAMIKO KUHUSU MAOMBI YA DELIVERANCE
Kumekuwa na malalamiko kadhaa kutoka kwa baadhi ya waumini wa Kikristo nchini wakilalamikia maombi ya deliverance yanayofanywa na baadhi ya wachungaji, wengine wakisemekana kutumia nafasi hiyo kuzini na wake za watu.
Maombi hayo yanayofanywa na baadhi ya watumishi wa Mungu, hupewa kipaumbele cha muombewa na mwombaji kuwa wawili tu, wakati mwingine hufanyika nje ya kanisa kama hotelini au gesti!
CHANZO:GPL
0 Comments