Akiwa bado kwenye majonzi makubwa ya mkewe aliyefariki duniani mwanzoni mwa mwezi huu, beki wa zamani wa Manchester United na timu ya Taifa ya England Rio Ferdinand ameweka wazi mikakati yake mipya katika mahojiano aliyoyafanya.
Mchezaji huyo ambaye kwa sasa ana miaka 36 ametangaza nia ya kustaafu soka baada ya klabu ya Queens Park Rangers kutangaza kumtema kwenye kikosi chake.
Rio Ferdinand akiwa na marehemu mkewe Rebecca
Alitangaza uamuzi wake katika mahojiano ya moja kwa moja na BT Sport, na aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter kuwashukuru waliomtakia kila la heri baada ya kifo cha mkewe, Rebecca aliyekuwa akisumbuliwa na maradhi ya saratani, ambaye wamezaa naye watoto watatu.
Ferdinand hakuacha kumsifia kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson kwamba ni mfano wa kuigwa kutokana na ujuzi wake.
Manchester United ilitoa Pauni Milioni 30 kumnunua Ferdinand Julai mwaka 2002 na kumfanya awe beki ghali katika historia ya soka ya Uingereza wakati akisajiliwa kutoka Leeds United.
0 Comments