Mbunge wa Chalinze, mkoa wa Pwani, Mtoto wa Rais, Ridhiwani Kikwete, akijaribu kimoja kati ya vitanda 267, kabla ya kuvigawa kwa shule saba za jimboni Chalinze, katika hafla iliyofanyika jana, kwenye shule ya Sekondari Lugoba jimboni humo. Shule zilizopewa vitanda hivyo vikiwa na magodoro yake, idadi ya vitanda ilivyopata ikiwa kwenye mabano ni; Chalinze (50), Moreto (50), Mandera (25), Talawanda (24), Kiwangawa (50), Lugoba (38) na Kikaro (30). Kwa mujibu wa Ridhiwani mgawo huo ni wa awamu ya kwanza.
Ridhiwani akimkabidhi vitanda 50 Mwalimu Emmanuel Kahabi kwa ajili ya shule ya Chalinze. Kushono ni Abubakari Mlawa wa Kampuni ya MM Steel iliyotoa vitanda hivyo
Abdalla Sakasa wa Lugoba- akikabidhiwa vitanda vitanda 38
Charles Mussa wa Talawanda- vitanda 24
Justin Nguma wa Moreto vitanda 50
Omari Msami wa Kikaro-vitanda 30
Rose Umila wa Mandera Girls vitanda 25
Saidi Ally wa Kiwangwa akipongezwa na wadau baada ya kupata vitanda 50.
Ridhiwani akifurahi na wanafunzi wa shule ya Talawanda baada ya kukabidhi vitanda kwa mwalimu wa shyle hiyo (kulia)
Mgawo awamu ya kwanza
Ridhiwani akizungumza na wadau kueleza mikakati mbalimbali ya kukwamua maendeleo ya jimbo la Chalinze, ambapo alieleza kuwa miongoni mwa vipaumbele ni huduma za umeme ambapo italetwa Transfoma itakayowezesha jimbo hilo kupata umeme wa uhakika, afya na elimu
Wadau wakimsikiliza Ridhiwani. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO-CCM Blog
0 Comments