MKAZI wa kitongoji cha Temeke kilichopo katika Mtaa wa Nanjoka mjini Tunduru Mkoani Ruvuma, Maimuna Omari (62) aliyeripotiwa kufariki Dunia na kurejea katika Uzima (Kufufuka) Juni 16 mwaka huu afariki tena.
Tukio hilo ambalo limeonekana kuvuta hisia za watu na kufanya Mamia ya wakazi wa kitongoji na mjini wa Tunduru kwa ujumla kujitokeza kujionea maajabu hayo ya Mwezi mungu baada ya mtu huyo kufa kwa mara ya pili.
Wakizungumzia tukio hilo Watoto wa mama huyo Bi. Fatuma Yusuph na Bw. Seremani Yusuph walisema kuwa safari hii kifo cha mama yao kilichotokea July 9 mwaka huu kimedhibitishwa na Wataalamu kutoka katika Hospitali ya serikali ya Wilaya ya Tunduru alikokuwa amalezwa ikiwa ni tofauti na awali ambapo walitumia wazee maarufu na mashekhe katika mtaa huo.
Walisema baada ya tukio hilo kudhibitishwa walipeleka taafa za msiba huo Nyumbani kuwaita rafiki zake Bi.Fatuma Mohammed,Fatu Mbwana na Bi. Zainabu Siyabu kwa ajili ya kutekeleza madhehebu ya Dini ya kiislamu yanayo waelekeza kuwa baada ya kifo inapaswa marehemu kupatiwa maji na kumkamua kwa ajili ya kumtoa kinyesi (KUMKAFINI) ambayo akina mama hao na kuyafanya bila kikwazo chochote.
Wakizungumzia tukio la kwanza walisema kuwa Juni 16 mwaka huu mama yao huyo alifariki dunia akiwa nyumbani kwake majira ya saa 6.00 za usiku na baadae kurejea katika uzima majira ya Saa 4.30 asubuhi wakati wakiwa katika matarajio ya kwenda kumpuzisha katika nyumba yake ya milelel saa 7 za mchana wa siku hiyo.
Walisema kifo hicho kimetokea baada ya Mama yao huyo kuugua kwa muda murefu hali ambayo iliwakatisha tama wanafamilia hao hali ambayo iliwalazimu kumtoa hospitali ambako alilazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu na kumrejesha nyumbani kwa matazamio ya Ugonjwa huyo kutopona.
Wakizungumzia tukio hilo kwa nyakati tofauti Mtendaji wa Kijiji hicho Bi. Zidaya Halifa na Mjumbe wa mtaa huo Bw. Chimwaga Bakari Chimwaga na kwamba maraehemu anatarajiwa kuzikwa majira ya Saa 7 .00 za mchana katika makaburi yaliyopo katika eneo la Shule ya Msingi Umoja mjini hapa.
0 Comments