Header Ads Widget

HII NI NOOUMA!!: ETI BINTI KAKUTWA KALALA KWENYE KABATI LA CHIPS HUKO YOMBO JIJINI DAR



Hili tukio waweza fikiri ni uongo,hii ni kweli kabisa mrembo mmoja amekutwa amelala kwenye kabati la chips maeneo ya Yombo Vituka jijini Dar es salaam leo asubuhi.

Imeelezwa kuwa jana usiku Muuza chips alipofunga kabati na kufunga eneo lake la biashara kwa kufuli kisha akaenda kulala.

Walioshuhudia tukio hilo wanasema muuza chips alipofungua leo alimkuta mwanadada huyo ambaye hakujulikana jina lake akiwa amelala fofofo juu ya chips na mishikaki akiwa hajitambui

Hata hivyo bado haijajulikana aliingiaje kwenye kabati hilo la chips maana hakuweza kuongea baada ya kutolewa katika kabati hilo

Post a Comment

0 Comments