Kama ulikuwa hujui ngoja nikufahamishe, Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa huko nchini Uingereza umebaini kuwa kulala chumba chenye mwanga uliopitiliza kumehusishwa na mtu kuongeza unene wa kupindukia.
Timu ya watafiti kutoka Taasisi ya saratani ya jijini London imebaini kuwa wanawake wana nafasi kubwa ya kuongezeka unene kwa kulala vyumba vyenye mwanga mkubwa.
Hata hivyo utafiti huo unaonya kuwa hakuna ushahidi wa kutosha kuwa sasa watu waanze kununua mapazia mazito au ulazima wa kuzima taa wakati wa kulala.
Sasa jiulize kibongobongo hii imekaaje kutokana na mazingira ya nyumba zetu?
0 Comments