Header Ads Widget

HUYU NDIYE KIJANA ANAYETAKA KURUSHA NDEGE DUNIA NZIMA AKIWA PEKE YAKE.



Vijana wengi wenye umri wa miaka 19 wanajipanga kwa ajili ya likizo ya majira ya joto. Lakini ni tofauti wa kijana Matt Guthmiller kutoka jijini Las Vegas nchini Marekani anatarajia kutumia likizo yake hiyo kwa kurusha ndege dunia nzima akiwa yeye mwenyewe yani peke yake.



Guthmiller anatarajia kurusha ndege ya 1981 Beechcraft A36 Bonanza kwa matarajio ya kuwa rubani wa kwanza mwenye umri mdogo kurusha ndege dunia nzima peke yake.

Anasema ameguswa na kijana mwenye umri wa miaka 21 Jack Wiegand ambaye alikamilisha safari yake ambapo sasa anashikilia rekodi ya kitabu cha Guinness.



Safari hiyo inatarajia kufanyika kwa takribani siku 40 au saa 160 za kusafiri angani ingawa anapanga kusimama katika vituo 20 katika mabara matano na kuweka kila anachokifanya katika mitandao ya kijamii. Ingawa rubani huyo mdogo mipango yake ni kupata nafasi katika kitabu cha rekodi za dunia, Guthmiller anasema safari yake hiyo itawahamasisha vijana wengine kufuata ndoto zao.

Post a Comment

0 Comments