
Tuzo za watu za Tanzania au Tanzania People's Choice Awards zitatolewa leo kwenye ukumbi uliopo Serena Hotel jijini Dar es Salaam.
Jumla ya vipengele 11 vinashindaniwa na nominee watatu katika kila kimoja wameingia fainali.
Mshindi katika kila kipengele atapewa zawadi ya shilingi milioni moja pamoja na trophy.
Host wa tuzo hizi ni mtangazaji mkongwe wa radio, Jimmy Kabwe.
Pamoja na burudani mbalimbali zitakazokuwepo, video mpya ya Ben Pol ya wimbo wake ''Unanichora'' aliomshirikisha Joh Makini itazinduliwa.
0 Comments