Kaimu kamanda wa polisi mkoa Morogoro John Laswai amesema tukio la kwanza limetokea eneo la Mtawala Msamvu ambapo mwendesha pikipi na abiria wake waliingia chini ya lori na kufariki papo hapo, na tukio jingine lilimeetokea eneo la Kihonda barabara ya Morogoro Dodoma ambapo lori liligongana na kenta na kumbana dereva miguu ambapo alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu na chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi.
Kwa upande wao mashuhuda wa ajali hizo wakiwemo majeruhi wamekiri chanzo cha ajali hizo ni uzembe wa madereva na kuomba mamlaka husika kusimaia sheria za barabarani ili kupunguza matukio ya jali zinazogharimu maisha ya watu kwa kusababisha vifo na vilema vya kudumu.
Marehemu wote wametambulika na miili imehifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospitali ya mkoa wa Morogoro.
0 Comments