HOME
KUHUSU BLOGU
MAWASILIANO YETU
TANGAZO
Header Ads Widget
30%More Salary
'The season to Switch Job!
Join Now
High Paying Jobs
These styles are going quick.
Join Now
50% Reputed Companies
Only while Vacancies Are Left.
Join Now
MWANZO
HABARI
NAFASI ZA KAZI
KUKAYA MIONO
MICHEZO
TIBA MBADALA
MAHUSIANO
MIONO TV
RIWAYA
Home
Tiba mbadala
HIZI NDIO DALILI ZA MWANAMKE ZITAKAZOMFAHAMISHA OVULATION/SIKU ZAKE ZA HEDHI ZIMEWADIA .SOMA NI MUHIMU
HIZI NDIO DALILI ZA MWANAMKE ZITAKAZOMFAHAMISHA OVULATION/SIKU ZAKE ZA HEDHI ZIMEWADIA .SOMA NI MUHIMU
Kwetu Miono
12:14:00 AM
OVULATION ni hali ya kutoka kwa yai la kike baada ya kukomaa kutoka kwenye follicle baada ya kukua na kukomaa katika ovary. Hali hii hutokea katika hali ya kawaida katika siku ya 14 katika mzunguko wa siku 28.
Alama/dalili hizo
za Ovulation si ngumu kuzitambua, iwapo
utafahamu unatafuta alama gani. Kuna
baadhi ya alama za mwili
zinazokutahadharisha kwamba Ovulation
iko njiani, hivyo kuweza kukusaidia
kupanga vyema muda wa kujamiiana kwa
ajili ya kupata mimba.
Alama/ dalili nyinginezo
zinakufahamisha kwamba Ovulation
imewadia au imeshapita. Ingawa alama hizo
ziko nyingi na nitazungumzia baadhi ya
hizo, lakini usifikiri kwamba unatakiwa
utumie zote, kwani kufanya hivyo kunaweza
kukuchanganya.
Iwapo hutoona alama zozote za Ovulation
au iwapo siku zako za mwezi hazina
mpangilio maalum, ni bora umuone daktari
ambaye atakusaidia zaidi.
1.Mabadiliko ya joto lako la Mwili
Tunaweza kusema kuwa Joto lako la mwili
au (Body Basal Temperature) ndio alama/ dalili
maarufu inayotumiwa na wanawake wengi
ili kufahamisha kwamba Ovulation
imewadia pale wanapotaka kubeba mimba.
Hii ni kwa sababu joto lako la mwili
huongezeka kwa kiasi kidogo na huendelea
kuongezeka baada ya Ovulation. Ongezeko
hilo la joto husababishwa na homoni ya
progesterone, ambayo huongezeka sana
punde baada ya Ovulation.
Kwa kujipima
joto lako la mwili na kuandika chati ya
mabadiliko hayo unaweza kufahamu
ongezeko hilo la joto lako la mwili.
Unahitajia kipimamoto kwa ajili ya
kufanikisha suala hilo. Zipo pimajoto
maalum kwa ajili hiyo lakini unaweza
kutumia pimajoto ya kawaida pia. Hakikisha
unapima joto la mwili wako asubuhi baada
ya kuamka na uhakikishe huna homa,
hukukosa usingizi, hukunywa pombe, si
mgonjwa wala huna wasiwasi na fikra
nyingi. Ni bora ufanye hivyo kwa mizunguko
kadhaa ya siku zako ili uweze kuijua vyema
chati ya mabadiliko ya joto la mwili kwa
mujibu wa mzunguko wako wa mwezi.
Ingawa njia hii haiainishi moja kwa moja
kuwa Ovulation imewadia, lakini joto la
mwili huongezeka kidogo kabla ya kipindi
hicho na huongezeka kwa kwa degree 0.4
hadi 0.6 baada tu ya kumalizika Ovulation.
Kuongezeka joto kwa kiasi kikubwa baada
ya Ovulation huendelea hadi siku
utakayopata siku zako ambapo hupungua
na mzunguko wako wa mwezi huanza tena.
Iwapo utakuwa umepata mimba joto lako la
mwili litaendelea hivyo hivyo kuwa juu.
Kwa
kuwa mabadiliko ya joto hutokea wakati wa
Ovulation iwapo unajaribu kubeba mimba,
kufuatilia mabadiliko hayo kwa muda
usiopungua miezi miwili ni jambo la
dharura ili uweze kujua wakati wa Ovulation
ambapo una uwezekano mkubwa wa
kubeba mimba.
2.Mabadiliko ya majimaji ya ukeni
Wakati Ovulation inakaribia majimaji ya
ukeni hubadilika pia kwa kiasi na hali. Ikiwa
hakuna Ovulation majimaji ya ukeni huwa
yanayonata au kama kremu au hukosekana
kabisa. Wakati Ovulation inakaribia majimaji
ya ukeni huongezeka na huwa katika hali ya
majimaji na wakati mwingine huwa rangi
nyeupe kama ya yai bichi. Iwapo utapima
kwa vidole vyako huvutika kwa inchi au
zaidi kati ya vidole vyako.
Ni bora nikumbushe hapa kwamba, kuangalia
wakati unaweza kuwa na majimaji ya ukeni
yanayofanana na ya wakati wa Ovulation
hali ya kuwa huko katika Ovulation. Hali hiyo
ni ya kawaida kwa watu wenye PCOS.
Kutumia dawa za Clomid au Antihistamin
huweza kufanya majimaji ya ukeni yakauke
na hivyo kuwa vigumu kutumia njia hii ili
kujua ni zipi siku zennye uwezekano
mkubwa wa mimba. Njia hii huhesabiwa
kuwa yenye itibari zaidi.
3.Ongezeko la Matamanio
Inaonekana kuwa maumbile nayo
hutusaidia kujua ni siku gani tunaweza
kubeba mimba! Wataalamu wameonyesha
(jambo ambalo pengine wengi
wameshalihisi) kwamba wanawake
wanapokuwa katika siku zenye uwezekano
mkubwa wa kupata mimba, matamanio yao
ya kufanya mapenzi huongezeka. Hizo ni siku chache
kabla ya
kujiri Ovulation, ambapo ndio wakati
unaofaa wa kujamiiana iwapo unataka
kubeba mimba.
Hata hivyo njia hii si ya kutumainiwa sana
kwani baadhi ya hali kama vile
msongamano wa mawazo, fikra nyingi na
wasiwasi huweza kupunguzaa matamanio.
Au mtu anaweza akahisi matamanio katika
muda wote wa mzunguko wa mwezi.
4.Mabadiliko ya Ukeni:
Kama ambavyo majimaji ya ukeni
yanavyobadilika wakati wa Ovulation, uke
nao (cervix) hubadilika wakati wa kukaribia
Ovulation. Wakati huo uke husogea mbele,
huwa laini na hufunguka zaidi.
5.Maumivu kidogo katika Matiti:
Baadhi ya wanawake wakati wanapokaribia
Ovulation au baada ya hapo matiti yao huwa
na maumivu kidogo. Suala hili huhusiana na
mabadiliko ya homini mwili ambazo
hujitayarisha kwa ajili ya mimba. Hata hivyo
njia hii sio yenye kutegemewa sana kwani
maumivu ya matiti huweza kusababishwa
na masuala mengine. Pia maumivu ya matiti
hutokea kabla ya hedhi au baada ya kutumia
baadhi ya dawa za kusaidia uzazi.
Alama/ dalili nyinginezo
Baadhi ya wanawake huhisi maumivu
kidogo ya tumbo ambayo baadhi huyaita
Middle Pain. Maumivu hayo kwa kawaida
hutokea upande ule yai linapotoka yaani
upande wa Ovulation. Maumivu hayo
hutokana na mwendo wa yai wakati
linapopenya kwenye mirija. Maumivu hayo si
ya kuendelea na wala si makubwa na huisha
haraka. Hali hiyo huweza kutokea mara
kadhaa katika siku za Ovulation.
Kuna
baadhi ya alama kama vile baadhi ya
wanawake huhisi kichefuchefu, gesi,
kukojoa mara kwa mara na maumivu wakati
wa kujamiina, hali ambayo haitokei kwa
watu wengi. Pia kuna baadhi ya vifaa
vinavyopaatikana katika maduka ya dawa
katika baadhi ya nchi ambavyo huweza
kukusaidia kujua wakati wako wa Ovuation
umewajia, vifaa hivyo hujulikana kama
'Ovulation Kit"
La muhimu ni kufahamu kuwa wanawake
hutofautiana katika kupata alama hizi,
kwani kuna baadhi wanaweza wakapata
baadhi ya alama hizi na wengineo wakapata
nyinginezo. Kuuelewa vyema mwili wako ni
jambo zuri linaloweza kukusaidia kuzijua
siku zako la Ovulation na hivyo kuweza
kujua siku zako za kubeba mimba.
Post a Comment
0 Comments
FUATILIA MITANDAO YETU YA KIJAMII
PATA PESA MTANDAONI BOFYA TANGAZO
SUBSCRIBE CHANNEL YETU HAPA.
HABARI MPYA
Kukaya Miono
Ujenzi wa Boma la Darasa shule Ya Msingi Miono wakamilika bado kupaua
Kwetu Miono
10:18:00 AM
WASILIANA NASI HAPA KWA CHOCHOTE BOFYA TANGAZO
ZILIZOSOMWA ZAIDI
ETI HIZI NDIYO SABABU ZINAZO PELEKEA WANAUME WENGI WA KITANZANIA KUPENDA WANAWAKE WENYE MAKALIO MAKUBWA NA MALAINI NI HIZI HAPA:
7:10:00 AM
Baada ya David Beckham kusikia kuwa Zidane ameteuliwa kuwa kocha wa Real Madrid, haya ndio aliyoandika …
10:34:00 PM
MAMBO YA KANGA MOKO HAYA HAPA.
4:17:00 AM
Yanga Yashindwa kutamba uwanja wa taifa Zidi ya AlAhly Dsm April 9 2016 +Video
9:23:00 AM
Video: Polisi Walazimika Kutumia Mabomu Kuwatawanya Wafanyakazi wa Kiwanda cha Pepsi
11:30:00 PM
UNAAMBIWA KONDOM ZA MALAYA WANAOJIUZA MKOANI MOROGORO ZAWAATHIRI WATOTO..MKUU WA MKOA AJITOA KUZUNGUMZIA HILO AKISEMA HADHI YAKE HAIMRUHUSU KULIONGELEA SUALA HILO
9:16:00 AM
Sasa Wasanii Bongo kulipwa kwa nyimbo zao kuchezwa kwenye Tv na Radio? majibu anayo Waziri…(+Video)
6:07:00 AM
JUMLA YA WATEMBELEAJI WETU
6
4
1
5
1
2
JIUNGE NASI KWENYE FACEBOOK.
Contact form
0 Comments