Header Ads Widget

Watu 101 waliofariki kutokana na mvua kubwa na mafuriko Nchini Somalia

Watu 101 waliofariki kutokana na mvua kubwa na mafuriko Nchini Somalia

Idadi ya watu waliofariki kutokana na mvua kubwa na mafuriko nchini Somalia imeongezeka hadi 101 huku watu milioni 1 wakiwa wamekimbia makazi yao na milioni 1.5 wameathiriwa nchini kote.

Hayo yamedokezwa na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud katika hotuba yake kitaifa kwa njia ya televisheni. Amebaini kuwa Somalia inakabiliwa na mzozo wa kibinadamu unaosababishwa na mvua kali za tukio la El Nino.
Alisema mafuriko hayo pia yameua mifugo 4,000 na kuharibu nyumba 140,000.
Mohamud alisema kuwa kwa miaka 16 iliyopita, kundi la kigaidi la al-Shabaab limezuia uwezo wa watu wa kulima na kuvuna na limekataa kuruhusu mashirika ya kibinadamu kusaidia watu katika maeneo wanayodhibiti.

Ameongeza kuwa kwa uungwaji mkono wa jumuiya ya kimataifa na mashirika ya misaada, baa la njaa liliepukika mwaka 2022 jambo ambalo lingekuwa janga kwa zaidi ya watu milioni 7.7 nchini humo.

Post a Comment

0 Comments