Header Ads Widget

Manchester Utd Bado Ina Nafasi Ya Kufuzu 16 Bora

Manchester Utd Bado Ina Nafasi Ya Kufuzu 16 Bora

Nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes, alikuwa na kiwango bora sana usiku wa mabingwa Ulaya kwenye mchezo uliomalizika kwa sare ya 3-3 dhidi ya Galatasaray ugenini.

Man United walikwenda kwenye mchezo wakiwa na matumaini ya kupata pointi tatu na walianza vizuri wakiongoza 2-0 baada ya dakika 18 tu.

Fernandes alitoa pasi ya ufunguzi kwa Rasmus Hojlund dakika ya 11, na dakika saba baadaye, yeye mwenyewe alifunga mojawapo ya mabao bora katika hatua ya makundi. Unaweza kubashiri ni mchezaji gani atafunga goli, chaguo hili lina odds kubwa Meridianbet.

Mreno huyo alipiga shuti kali nje ya 18 na kufunga goli bora huku Fernando Muslera hakuwa na nafasi ya kuzuia shuti hilo. 

Ilionekana kama walikuwa kwenye njia ya ushindi wa kutosha, lakini mchezo ulimalizika 3-3 baada ya filimbi ya mwisho. Andre Onana alifanya makosa mawili kutokea kwenye mipira miwili ya adhabu ya Hakim Ziyech

Fernandes alifanya madhambi yaliyosababisha magoli mawili ya Ziyech, lakini hana la kulaumiwa kwenye hilo. Je nafasi ya Utd kufuzu hatua ya 16 bora ipo kwa kiasi gani, 

Bruno Fernandes mwenye (29) mbali na mchango wake wa mabao mawili, aligusa mpira mara 60 na kutoa pasi tatu muhimu pamoja na pasi nne ndefu. 

Fernandes pia alishinda mipira 5 ya kugombania na kufanya tackling 3, lakini haikutosha kuleta ushindi muhimu kwa Man United kwenye usiku wa mabingwa.

United walipoteza faida ya 2-0 kwa mara nyingine msimu huu. Matokeo haya yanawafanya kuwa chini ya kundi lao na pointi 4 na wanakabiliwa na uwezekano wa kutolewa.

Galatasaray na Copenhagen wana pointi 5 kila mmoja. United wanahitaji kushinda dhidi ya Bayern Munich na kuomba mchezo mwingine umalizike kwa sare.

United lazima ikomeshe Unbeaten ya Bayern kwa mechi 39 katika hatua ya makundi ili kuwa na nafasi ya kufuzu raundi ya 16 ya Ligi ya Mabingwa. Je Man Utd wataweza kuifunga Bayern?

Post a Comment

0 Comments