Header Ads Widget

Moses Phiri Afunguka Kurejea Kikosi Cha Kwanza Simba

Moses Phiri Afunguka Kurejea Kikosi Cha Kwanza SimbaMoses Phiri

Moses Phiri Aamua Kuvunja Ukimya Simba Kurejea Kikosi Cha Kwanza

MSHAMBULIAJI wa Simba, Moses Phiri amesema kuwa licha ya changamoto ya nafasi ya kucheza anayoipata katika timu hiyo lakini bado anaamini atazidi kupambana na kurejea kikosi cha kwanza cha Simba.

Phiri amekuwa akikosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo licha ya kuonyesha uwezo mkubwa mwanzoni mwa msimu uliopita ambapo Simba walimsajili mchezaji huyo kutokea Zanaco ya Zambia.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Phiri alisema kuwa anafahamu changamoto kubwa ambayo ipo kwake ni kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza kutokana na ushindani wa namba kuwa mkubwa ambao upo katika kikosi hiko lakini bado anaamini kuwa atafanya vyema pindi akipewa nafasi ya kucheza.
“Naaamini kwa sasa katika kupambana ili nipate nafasi ya kucheza na wala sio jambo lingine, ndani ya kikosi kwa sasa kuna ushindani mkubwa wa nafasi kwa maana ya kila mchezaji ni mzuri na anataka kucheza ili kuweza kuisaidia timu.

“Sasa kikubwa kwa upande wangu pale ambapo nitapata nafasi basi nizitumie vyema ili niendelee kumshawishi mwalimu aweze kunipa nafasi zaidi ili niweze kuwa sehemu kubwa ya mchango kwa timu hii,” alisema mchezaii huyo

Post a Comment

0 Comments