Burkina Faso na Mali kwa pamoja zimewaonya Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) kwamba wakithubutu kuvamia Nchi ya Niger ili kuwakabili Wanajeshi waliompindua Rais wa Nchi hiyo basi itakuwa ni sawa na kutangaza vita na Nchi hizo pia na hawatosita kupigana ili kuwasaidia Wanajeshi wa Niger.
Kauli ya Burkina Faso na Mali inakuja siku moja tangu ECOWAS itishie kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya utawala wa Niger baada ya kumpindua Rais wa Nchi hiyo Wiki iliyopita ambapo ECOWAs iliwapa siku saba Wanajeshi wamrejeshe madarakani Rais aliyepinduliwa Mohamed Bazoum ambaye anashikiliwa mateka.
Burkina Faso na Mali ambazo pia zinatawaliwa Kijeshi baada ya mapinduzi, kwenye taarifa yao ya pamoja wamesema “Serikali zetu za mpito zinaunga mkono Waniger ambao wameamua kujikomboa wenyewe na kuchukua Mamlaka yao”
“Uvamizi wowote wa kijeshi kwa Niger itakuwa ni sawa na kutangaza vita kwa Burkina Faso na Mali pia na itapelekea machafuko ambayo yatauletea shida ukanda mzima, na hatutaki kushiriki kuiwekea vikwazo visivyo halali Niger”
0 Comments