UNAAMBIWA sasa ni rasmi kuwa mshahara wa milioni 50 aliopewa Fiston Mayele unamhalalisha hatakuwa mchezaji tena wa Yanga msimu ujao baada ya kuomba kwenda kukipiga nchini Saudi Arabia huku Yanga wakilambishwa zaidi ya Bilioni 1.2 kama dau la usajili.
Mayele alijiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili kisha akaongezwa mmoja mwaka jana akitokea As Vita ya DR Congo.
Wakati Mayele akijiandaa kusepa, tayari Yanga wameshaanza kusaka mbadala wake na jicho lao limeangukia kwa straika mwili jumba, Sudi Abdallah raia wa Burundi.
Chanzo chetu cha uhakika kimeliambia Championi Ijumaa kuwa, Yanga wamewekewa mezani dola laki 5 (Sh bil 1.2) kama fedha ya kununua mkataba wa mwaka mmoja uliosalia kwa Mayele.Straika mwili jumba, Sudi Abdallah raia wa Burundi.
Mbali na hapo, Mayele mwenyewe amepewa Sh Milioni 400 kama fedha ya usajili na mshahara wa dola elfu 25 (Sh mil 60.7) kila mwezi.
“Kwa sasa ninaweza kukuhakikisha kabisa kuwa, Mayele anaondoka kwetu na ataenda kucheza huko Saudi Arabia ambapo amepata moja ya timu na imempa zaidi ya mshahara wa Sh mil 60 kila mwezi.STRAIKA MWILI JUMBA MLANGONI YANGA
“Mshahara huo umekuwa ni mkubwa kwetu hivyo tumeshindwa kumbakiza kwani pia wamempa dola 200,000 (Sh mil 486.1) kama sehemu ya usajili wake, huku kwetu wakitupatia hiyo zaidi ya Bilioni moja ili tumuachie,” kilisema chanzo hicho.
AMINI usiamini Sudi Abdallah, ambaye ni raia wa Burundi, ndiye straika mpya anayekuja Yanga kurithi mikoba ya Mayele anayeondoka kwenda kucheza kwenye moja ya klabu huko Saudi Arabia.
Sudi mara ya mwisho Januari 12, 2023, aliuzwa na Klabu ya Al-Naft SC ya nchini Iraq ambapo Julai 5 alijiunga na Klabu ya Kuching City ya nchini Malaysia inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo.
Chanzo chetu kutoka Yanga kimeliambia Championi Ijumaa kuwa, baada ya uongozi wa Yanga kukosa matumaini ya kumpata Mayele, waliamua kuingia mawindoni kisha wakamnasa mwamba Sudi Abdallah aliyekuwa na ufalme wa kutosha nchini Iraq.
“Tunamshukuru Mungu kwa kutupatia mbadala wa Mayele, ambapo sasa msimu ujao tuna uhakika tena wa kwenda kutamba na bonge la straika wa mabao na mkali wa kuchana nyavu.
“Jamaa amekubali kujiunga kwetu kwa dau la milioni 400 tu huku kila mwezi akiomba mshahara wa milioni 25, fedha ambayo ni nafuu zaidi kwetu baada ya kushindwa kumbakiza Mayele,” kilisema chanzo hicho cha kuaminika kabisa
0 Comments