Header Ads Widget

Kocha Wa Yanga Apigia Saluti Usajili Wa Ngoma Simba

Kocha Wa Yanga Apigia Saluti Usajili Wa Ngoma SimbaFabrice Ngoma

KOCHA wa zamani wa Yanga na AS Vita, Roul Shungu, amefunguka kuwa, kitendo cha Simba kufanikiwa kumpata aliyekuwa kiungo wa Al Hilal ya Sudan, Fabrice Ngoma, itawasaidia kuboresha safu ya kiungo ya timu hiyo kuelekea msimu ujao kutokana na kuufahamu vema ubora wa kiungo huyo.

Shungu ambaye kwa sasa anafundisha timu ya Taifa ya DR Congo chini ya miaka 20, ametoa kauli hiyo kufuatia Simba kutangaza kumsajili kiungo huyo kwa mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya msimu ujao ambao Simba mbali na michuano ya ndani, pia itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.Kocha Wa Yanga Apigia Saluti Usajili Wa Ngoma SimbaRoul Shungu

Akizungumza na Spoti Xtra, Shungu alisema anaona Simba imefanikiwa kupata mchezaji mkubwa, huku akimkingia kufua juu ya suala la kupata majeraha ya mara kwa mara hali inayopelekea kushindwa kudumu na timu moja kwa muda mrefu.
“Naona kwangu Simba imepata mchezaji mkubwa kwa sababu nafahamu uwezo wake maana amepita katika mikono yangu wakati akiwa AS Vita ingawa aliondoka kwenda Wydad Casablanca, kisha Al Hilal ambayo ipo chini ya Kocha Frolent Ibenge.

“Suala la majeraha siwezi kukubaliana nalo kwa sababu wakati nipo naye AS Vita alikuwa mmoja kati ya wachezaji muhimu, hakuwa na hiyo sifa ya majeraha ya mara kwa mara ambayo imekuwa ikitajwa,.

“Nimesikia hata Yanga waliamua kuachana naye kwa sababu ya jambo hilo, lakini siyo kwamba lina ukweli,” alisema Shungu.

Post a Comment

0 Comments