Header Ads Widget

Yanga Yaiua USM Alger Kwao huku ikikosa Ubingwa.

Yanga Yaiua USM Alger Kwao huku ikikosa Ubingwa.

Yanga yaiua USM Alger ikikosa ubingwa wa Kombe la shirikisho balani Africa inayosimamiwa na CAF 

Ndoto za Yanga kutwaa Kombe la Shirikisho zimefifishwa na mabao ya ugenini licha ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika fainali ya pili dhidi ya USM Alger.

Dar es Salaam. Yanga imeandika historia nyingine usiku huu kwa kushinda ugenini kwa bao 1-0 dhidi ya USM Alger ya Algeria katika mechi ya marudiano ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, lakini ikalikosa taji la kwanza la CAF kutokana na faida ya bao la ugenini kuwabeba Waalgeria.

Wenyeji ilitwaa taji hilo la kwanza kwao baada ya awali kushinda ugenini 2-1 na matokeo ya jumla kuwa sare ya 2-2, lakini kanuni ya bao la ugenini ikawapata taji hilo kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Julai 5, 1962 mjini Algers na Yanga iliupiga mwingi tofauti na ilivyocheza jijini Dar.

Kocha Nasreddine Nabi aliwatumia mabeki watano, ikiwamo Dickson Job kama kiungo namba sita na kuwabana wenyeji na kufanikiwa kupata bao hilo pekee dakika ya saba tu likiwekwa kimiyani kwa penalti na beki Djuma Shaban baada ya Kennedy Musonda kuchezwa madhambi.


Post a Comment

0 Comments