Hatimaye Mahakama ya Moshi Mkoani Kilimanjaro mchana huu imetangaza kumuachia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya baada ya muda mfupi uliopita kukiri makosa yake yaliyokuwa yakimkabili.
Sabaya amekiri makosa yake kwa njia ya ‘plea bargaining’ ambao ni mchakato wa makubaliano/maridhiano maalumu katika kesi ya jinai kati ya Mwendesha Mashtaka na Mshitakiwa ambapo Mshitakwa anaweza kukubali kukiri kosa moja au zaidi katika makosa aliyoshitakiwa nayo ili apate nafuu katika kesi inayomkabili.
Taarifa kamili kuhusu kuachiwa kwake na maagizo ya Mahakama nitakupatia hivi punde.
0 Comments