Header Ads Widget

Waziri Mkuu Majaliwa asema bungeni, ‘Ajira 547,031 Mwaka 2022/2023



Serikali imeendelea kuratibu masuala ya uzalishaji wa fursa za ajira nchini kupitia utekelezaji wa miradi ya kielelezo, kujenga mazingira wezeshi kwa wawekezaji na kuimarisha ushirikiano baina ya Serikali na sekta binafsi ambapo katika mwaka 2022/2023, jumla ya fursa za ajira 547,031 zilizalishwa.

“Kati ya hizo, ajira 321,363 zilizalishwa kupitia Serikali na utekelezaji wa miradi ya maendeleo na 225,668 kupitia sekta binafsi”

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema hayo leo April 05,2023 Bungeni Dodoma wakati akisoma hotuba kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2023/2024.

“Serikali imeendelea kuchukua hatua ili kuhakikisha Wahitimu wa mafunzo ya ujuzi wanaunganishwa na fursa za kujiajiri, utaratibu huo utamwezesha Mhitimu wa mafunzo ya ujuzi kupata sehemu ya uzalishaji yenye viwango vinavyohitajika chini ya usimamizi wa Wataalamu wenye uzoefu katika fani husika kwa kipindi maalumu cha miezi 6 hadi 12 kutegemea na aina ya fani”

Post a Comment

0 Comments