KOCHA Mkuu wa Simba Mbrazil, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amepanga kuwapa nafasi wachezaji wote kwa lengo la kuangalia uwezo wa kila mmoja kabla ya kukabidhi ripoti ya kuwatema baadhi ya mastaa kuelekea msimu ujao.
Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, imepanga kukifanyia maboresho makubwa kikosi hicho katika msimu ujao kwa kusajili wachezaji wapya na kuwaongezea mikataba wale ambao inaelekea ukingoni.
Wapo baadhi ya wachezaji wanaotajwa kuachwa mwishoni mwa msimu huu wakiwemo viungo Augustine Okrah na Esmael Sawadogo ambao wameshindwa kuonyesha ushindani na kuingia katika kikosi cha kwanza.
Akizungumza na Championi Jumatano, Robertinho alisema amepanga kuwapa nafasi ya kucheza wachezaji wa akiba katika michezo ijayo ya Ligi Kuu Bara na Kombe la FA.
Aliongeza kuwa anataka kuona kila mchezaji anayepata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza anaonyesha kiwango bora kitakachomshawishi ambakishe katika msimu ujao.Roberto Oliviera ‘Robertinho’
Aliongeza kuwa tayari ana orodha ya wachezaji atakaowabakisha ambao wapo tayari katika kikosi licha ya mikataba yao kuelekea mwishoni, hivyo atakaa na uongozi kwa ajili ya kuwashawishi ili waboreshewe mikataba yao.
“Ninaamini uwezo wa kila mchezaji katika timu, lakini bado ninahitaji kuboresha kikosi changu kwa kuwapunguza baadhi na kuwasajili wengine wapya katika msimu ujao.
“Katika msimu ujao ninahitaji wachezaji watakaoendana na kasi, aina ya soka ambalo mimi ninalihitaji ili kuhakikisha ninakuwa na timu imara na tishio Afrika.
“Maboresho ni lazima niyafanye na hilo lipo wazi kabisa, timu yangu inapata nafasi nyingi za kufunga ambazo tunashindwa kuzitumia vizuri katika kufunga, hivyo ni lazima nisajili mshambuliaji mmoja mkubwa,” alisema Robertinho.
MATOKEO YA SIMBA CAF
Horoya 1-0 Simba
Simba 0-3 Raja
Vipers 0-1 Simba
Simba 1-0 Vipers
Simba 7-0 Horoya
Raja vs Simba?
0 Comments