Header Ads Widget

Manara Afunguka ya Moyoni Kwa Mkewe Mkubwa Baada ya Kusemekana Kaachana na Mke Mdogo "Wewe ni Wife Material"

Happy Relationship Anniversary to us.

Mkeka kwa My Rubi ❣️

Seven Years now toka tulipokutana kwa mara ya kwanza Dubai siku ya tarehe kama ya leo 10-1-2016, nilikuwa likizo ya mwisho wa mwaka,,ni muda sasa, nikawa kila siku nataka kukuoa lakini sijui nn kilinichelewesha?

Hatimae Mungu akapanga nikakuoa, umekuwa Mke bora na Mke mashuhuri ktk moyo wangu na kipenzi cha Watoto,Ndugu,na Wazazi pamoja na familia nzima, ukishabikiwa hadi na rafiki zangu wote.

Una exposure kubwa na unaijua dunia, Passport yako imenawiri mihuri, huna ushamba lakini hujidai, Una Utu na Utulivu, Una adabu na heshma,Una Upendo na Usikivu,sikumbuki kama ushawahi kutoa Saut kwangu ya ukali, na hata nikikosea kitu unajua lugha ya kuongea na Mumeo, kubwa kwako neno Sorry halina tabu, Sijui wapi niliteleza Buga mimi !! Lakini ndio kilimwengu hivyo.

Mke Mke Mashallah 🙏🏻🙏🏻
hata nilipokuolea Mke mwingine ,ukasema lau kama unafanya kidini nakuombea Mume wangu,,ukampokea mwenzio kilillah, hata Qatar kulipotokea changa moto kidogo, ukanifata kuniambia samehe Mme wangu, Sisi Wanawake na ukahakikisha furaha inarudi kwetu sote ( ntapata wapi Bugati mke wa aina hiyo )

Nafikiria zawadi ya kukupa Kwa leo katika siku yetu siioni itakayotosha, na uwezo wa kukunulia ndege sina, May be mkufu wa madini pendwa ya Gold wa kito cha Tanzanite iliyorutubishwa kwa 💎 walau itakufariji Sweetheart.

Wewe ni Pozo la maradhi yangu, hujawahi kugombana hata siku moja na mtu na tabasamu lako ni la kudumu, unawaheshimu hadi Madreva na Wafanyakazi wa nyumbani kwetu, Walinzi na Majirani Wote wanakufurahia, huna kiburi na Majivuno mke wangu.

Hata mtu akikukwaza mitandaoni hujibu my love, Una moyo wa Wanawake wa kizamani, umelelewa ukaleleka Mashallah, Watu wa mitandaoni wote wanakufurahia, Una Nyota darling.

Nakuomba nisamehe tena, Binadamu kukosea ni maumbile yetu Mke wangu 🙏🏻🙏🏻

Nakuombea pia Kwa Mungu ujifungue salama na tufurahie life.

I promise darling, utaenjoy na utafurahia ndoa yetu,

Seven years si haba 🙏🏻

Nb: My Posh Rubi,, unakuwa Mwanamke wa kwanza katiks maisha yangu kukuomba radhi hadharani, hope utaridhia Habibt , Sorry and love u forever.

Post a Comment

0 Comments