Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametangaza kwamba June 2016 mradi wa ujenzi wa barabara za Treni za kisasa za kusafirisha watu kwenye jiji la Nairobi utazinduliwa rasmi.
Taarifa niliyoidaka kupitia mtandao wa Nation ni kwamba serikali ya Kenya inashirikiana na nchi ya Hungary kwenye ujenzi wa mradi huu ambao utafanana na ule wa Addis Ababa Ethiopia ulioanza kufanya kazi September 2015.
Kwa ndani..
Miradi ya Treni kama hizi maarufu kwa jina la Tram ipo kwenye nchi zilizoendelea kama Hispania ambapo President Uhuru amesema shilingi bilioni 15 za Kenya zinatengwa kwa ajili ya hii shughuli ya kuondoa foleni kwenye jiji la Nairobi, jiji linalotajwa kuwa la kwanza kwa foleni Afrika Mashariki likifatiwa na Dar es salaam.
Treni ya Addis Ababa Ethiopia ilivyokua ikizinduliwa.
Ujenzi wa barabara ya Treni Ethiopia.
Barabara zitakazo husika kwenye mradi huu ni pamoja na Thika Superhighway, Ngong Road, Limuru Road na Ongata Rongai ambapo balozi wa Hungary Kenya amesema Treni hizo zitakua na uwezo wa kusafirisha abiria zaidi ya laki tatu kwa siku na itakua zaidi ya hiyo idadi iwapo matawi yote yatakamilika.
Hispania
TAZAMA HII VIDEO HAPA CHINI…
By Millard Ayo
0 Comments