Rais Magufuli Atinga Gwanda za Kijeshi, Arusha.
Amiri Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi wa Arusha Mjini wakati akipita Barabarani kuelekea Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli ambako pamoja na mambo mengine Leo Januari 23, anatarajiwa kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kundi la 57/15.
Rais Magufuli akiwa amevalia sare za kijeshi amesimamishwa na kuwasalimu wananchi katika maeneo ya Sanawali, Tekniko, Ngarenalo, Mbauda, Majengo na Kisongo.
By: Clouds fm
0 Comments