Hapa walikutana wakati wa mapumziko kwenye hili kongamano.
Hizi picha zake za Marekani kwa mujibu wa ripota wa TZA Kenya Julius Kepkoich, ni kwamba mmoja wa Waandaaji wa mkutano wa Brook Business uliowakutanisha pamoja marais wa afrika na wakuu wa kampuni za kimataifa ni mwimbaji Akon.
Akon mwenye asili ya Senegal aliezaliwa miaka 41 iliyopita ni miongoni mwa wakali wachache kutoka Afrika ambao waliweza kupenda na kuingia kwenye chati za muziki wa dunia. Pamoja na umaarufu na utajiri wake alioupata akiwa anaishi mpaka sasa nchini Marekani, Akon bado ameendelea kuikumbuka Afrika na hata kwenye baadhi ya interview zake na anachoandika kwenye mitandao ya kijamii, anasisitiza watu kuwekeza Afrika.
0 Comments