Wakazi wa Iringa wameifunga awamu ya kwanza ya Kilimanjaro Music Tour kwa kufurika katika uwanja wa Samora kushuhudia wakali wa muziki nchini wakitoa burudani bila kujali hali ya hewa ya baridi. Wakali kama Snura, Linex, AY, Mwana FA, Profesa Jay, Izzo Bizness, Joh Makini, Juma Nature, Mwasiti, Nikki wa Pili na Gnako Warawara walilishambulia jukwaa kwa masaa sita mfululizo na kuwakonga nyoyo maelfu waliojitokeza uwanja wa Samora kuwashuhudia. Ziara hiyo iliyozunguka mikoa mitano inatarajiwa kuendelea mwezi Agosti ikiwa ni kuupisha mwezi ramadhani na inatarajiwa kwenda mikoa ya Mbeya, Kigoma, Mtwara, Dodoma na kukamilishiwa Dar es Salaam.
Hizi ni baadhi ya picha toka katika uwanja wa Samora.
Dullah na Sam Misago wakifanya amsha amsha kwa kuwazadia mashabiki zawadi mbalimbali toka Kili.
Mama wa majanga snura akifungua show
Mama wa majana Snura na madansa wake wakiwa jukaani wakizindua show ya Kili Music Tour kwa kuonyesha umahiri wake wa kulishambulia jukwaa
Backstage: Rich Mavoko na Izzo Bizness
Mwasiti jukwaani huku akimpandisha na shabiki mmoja
Backstage: Linex
Backstage: Rich Mavoko akijiandaa kupanda jukwaani
Linex akilishambulia jukwaa
Rich Mavoko na madansa wake
Weusi
Mashabiki wakimuenzi mangwair
Mashabiki waliofulriko uwanjani
0 Comments