Licha ya kuwa na project iitwayo ‘Wema kwa Ubaya’, inayotarajiwa kuachiwa hivi karibuni, Linex aka Mjeda amesema amemshirikisha Diamond kwenye wimbo ambao anahisi utakuwa ni kwajili wa kwenda kimataifa zaidi. Akizungumza na Bongo5 leo, Linex amesema wimbo wake ‘Salima’ upo tayari na anamsubiria Diamond ili aangalie wanafanya video na director gani. “Kwa sasa nina kazi nyingi sana ndo maana hata ile project ya kuwatungia nyimbo watu imesimama kwa muda,” amesema. “Wema kwa Ubaya, ndo kazi ambayo ipo njiani kwa sasa lakini kuna wimbo nimefanya na Diamond unaitwa ‘Salima’, hii kazi itatoka baada ya Ubaya Kwa Wema, ni kazi ambayo ninaihitaji kufanya vitu vikubwa ndani yake ili
kwenda mbele zaidi. Kwahiyo namsubiria Diamond arudi alafu tutapanga video tunafanyiwa wapi, kama
ni nje ya Tanzania au hapa hapa tutajua. Lakini lengo langu kazi hii nataka ifike mbali zaidi, ipingwe
kwenye TV kubwa za Afrika na sehemu mbalimbali kwa sababu alipofika Diamond na sisi tunataka
tufike pia, ili wanapotajwa nje kama msanii wa Tanzania na sisi tuwepo,” aliongeza.
0 Comments