Header Ads Widget

UNAAMBIWA WANAUME WADAIWA KUTIMUA MBIO KABLA YA KUPOKEA MAJIBU YA VIRUSI VYA UKIMWI HUKO MKOANI KATAVI


WANAWAKE wengi wa Tarafa ya Mwese katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi, wanalazimika kujifungulia nyumbani kutokana na kunyimwa huduma kwenye kliniki baada ya kushindwa kwenda na waume zao kupimwa afya.

Hayo yalielezwa na Diwani wa Viti Maalumu, Thiodela Kisesa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani, akisema wajawazito wa tarafa hiyo wamekuwa wakikosa huduma ya kupimwa maendeleo ya afya zao kliniki kutokana na watoa huduma kuwakatalia wakitaka waende na waume zao.

Alisema wanaume wengi wamekuwa wakitakiwa kwenda na wake zao kupima afya ili kubaini mapema kama wameambukizwa virusi vya ukimwi (VVU) kuzuia vifo vya mama na mtoto.

Kisesa aliongeza kuwa kutokana na sharti hilo ambalo wanaume wanalikwepa, wajawazito wengi wamejikuta wakilazimika kujifungulia majumbani, hali ambayo inahatarisha uhai wa mama na mtoto.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Joseph Msemwa, alilieleza Baraza la Madiwani kuwa jukumu la kupimwa afya sio la mama peke yake, bali wote wawili na waume zao.

Alisema wapo wanaume wanaodhani kwamba mama akipimwa na kuonekana hana maambukizi ya VVU basi nao hawana, jambo ambalo alisema sio sahihi hata kidogo.

NA Walter Mguluchuma

Post a Comment

0 Comments